WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki, Mb (kulia) akiwasili katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kinondoni leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya
hiyo kuzungumza na Watumishi wa Umma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akimkaribisha Waziri Kairuki, na kushoto ni
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akizungumza na watumishi wa
umma wa wilaya ya Kinondoni leo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya
kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya hiyo
kuzungumza na Watumishi wa Umma, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Wilaya ya
Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya
hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bibi. Sixtha
Kevin Komba akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya
Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais-
Utumishi Bi. Leyla Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya maadili
katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es
Salaam.
Mstahiki
Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta (kulia) akitoa neno la
shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) baada ya kupokea hoja
za watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Pichani- Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na
kushoto ni Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli. Picha
na: Genofeva Matemu - MAELEZO
Waajiri
nchini wametakiwa kufanya uhakiki wa kina wa vyeti vya elimu kwa ajira
mpya zitakazotolewa ili kuwa na watumishi wa umma wenye sifa
zinazostahili katika utumishi wa umma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi
na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini
Dar es Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia sana kuepukana na kutojirudia
tena kwa suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.
“Jana
tumetoa vibali vya ajira 10,184 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na
Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma
waliobainika kughushi vyeti vya elimu, hivyo napenda niwasisitize sana
waajiri wote kufanya uhakiki wa kina ili tusiwe tena na watumishi wa
umma wasiostahili katika orodha ya malipo” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri
Kairuki amesisitiza kuwa zoezi la uhakiki ni endelevu ambapo lazima
lifanyika pale mtumishi wa umma atakaporudi katika kituo cha kazi kutoka
masomoni, na watakaorejea katika utumishi wa umma baada ya likizo bila
malipo au sababu nyingine.
“Tunafanya
hivi sio kwa nia mbaya, bali tunataka tuwe na watumishi wanaostahili
kuwepo katika utumishi wa umma kwa sababu wanaoghushi wanaziba nafasi za
wale wanaostahili kuwepo na wenye sifa katika utumishi wa umma” Mhe.
Kairuki aliongeza
Pia
amewataka Waajiri kusafisha taarifa wa watumishi wa umma mara kwa mara
katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
“Kuna
watumishi ambao muda wao wa kuwepo kazini umemalizika (wamestaafu)
lakini bado wanaendelea kuwepo, Mfumo wa HCMIS sasa kila ifikapo saa
06:01 usiku utakuwa unawaondoa wale wote ambao muda wao wa kuwepo kazini
umefika lakini bado wanaendelea kuwepo kwenye Mfumo.
Mhe,
Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam,
ambapo leo ni siku yake ya nne aliyoitumia kukutana na Watendaji na
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, baada ya
kuzungumza na watumishi wa umma wa Temeke na Mbagala.
Lengo
la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko,
ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili
kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma
nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-UTUMISHI
13.07.2017
No comments:
Post a Comment