UTUMIAJI WA VIPODOZI ASILIA UTALINDA NGOZI ZETU- IRENE
Na Julieth Mushi, MANYAMAJR.
Mtaalamu
na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi ametoa ushauri kwa
kina mama hususani wasichana kutumia vipodozi vyenye vimea asilia ili
kuepukana na kuharibu ngozi zao.
Amesema
hayo wakati akiongea na Manyamajr, Irene amesema kupitia saluni ya
Timeless wameweza kuwasaidia watu wengi na kuwapatia tiba kuhusiana na
masuala ya ngozi na hasa katika usahihi wa kutumia vipodozi
vinavyoendana na ngozi ya muhusika.
"Tunatoa
ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipodozi kulingana
na aina ya ngozi ya muhusika pia kutoa malekezo ya kutumia vitu sahihi
kwa wakati sahihi kama vile kulingana na hali ya hewa kipindi cha joto
na baridi,"amesema Irene.
Amesema
kuwa, anatoa ushauri kwa vijana hususani wa kike kujifunza zaidi
masuala ya urembo kwani inaweza kusaidia katika kuboresha ngozi zao na
wanaweza kutumia vipodozi sahihi na kutokuharibu ngozi zao.
Mbali
na kutoa tiba, Timeless walianza kutoa mafunzo rasmi mwaka 2016 Irene
amesema kuwa wanatoa mafunzo kwa vijana wanaopendelea kufahamu shughuli
mbalimbali za urembo ikiwemo tiba ya ngozi, upambaji ambapo wameweza
kutoa vijana wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na tayari wengine
wameshajiajiri katika sehemu zao na pia Timeless wanajishughulisha na
masuala ya kupamba maharusi, nywele na kucha na mapambo ya maharusi
ikwemo kadi.
Mtaalamu
na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akimuhudumia mteja
aliyetembelea katika banda lao la Timeless Hair and Beauty Saloon
kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na masuala ya urembo wa ngozi na kuonyesha baadhi ya mapambo ya maharusi yanayopatikana kwenye saluni yao ya Timeless.
Wateja wakiwa wanapata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Timeless Hair and Beauty Saloon katika banda laokwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment