TUNDU LISU AHOFIA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS) KUFUTWA
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula wa
wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa msimamo
wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.
Akizungumza jana kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema
mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria
kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao za sheria.
Alisema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na
katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria
kadri itakavyoona inafaa.
"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini,
tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka
msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa .
"Huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti
wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo linatakiwa kupingwa na
kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya" alisema Mh. Tundu Lissu.
Mbali na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa
kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi
haitokuwa na maana ya kuwepo kwa chama hicho.
MANYAMAJR:
No comments:
Post a Comment