TCAA yapiga marufuku kununua, kurusha ‘drones’ bila kibali maalum
Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa
vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali
maalum.
Kupitia
tangazo lake kwa umma, TCAA imesema kuwa kwa taasisi au mtu binafsi
kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya
Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.
“Ifahamike
kuwa kuanzia sasa, taasisi au mtu binafsi anayetaka kununua, kufanya
majaribio au kurusha angani vifaa hivyo visivyotumia rubani anapaswa
kupata idhidi ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na kibali kutoka
TCAA,” imeeleza taarifa ya Mamlaka hiyo.
Taarifa
hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua
kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka
hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Tangazo
hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa
na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kuchukua picha za juu,
pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa
yanapofanyika katika maeneo ya wazi.
Drones
zilitumika zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya
kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati
uliohudhuria.
No comments:
Post a Comment