Tabia Tano Muhimu Ambazo Ukizifuata Zitaboresha Maisha Yako Sana
Leo nataka tuangalie kupitia makala haya, tabia ambazo ukizifuata na kuzitekeleza zitafanya maisha yako kuwa bora na ya thamani kila iitwapo leo.
1. Usifanye kazi mbili kwa wakati mmoja.
Mawazo yako yote weka kwenye kitu kimoja unachokifanya. Ukiweka mawazo kwenye vitu viwili, utashindwa kuvifanikisha vyote kwa ufasaha na utashindwa.
2. Usigombane na mtu mpumbavu.
Kama kimetokea kitu cha kutoelewana na mtu ambaye unamwona hajielewi, achana naye ili asije akakupotezea muda wako bure.
3. Usiingie kwenye mabishano yasiyo ya lazima.
Fanya kile unachokiamini, kubishana kwingi na kujaribu kuonyeshana eti nani ni mshindi ni mambo ambayo yanapoteza muda wako pia. Epuka kubishana.
4. Usifanye maamuzi bila ya kufikiri sana.
Kama unataka kufanya maamuzi bora na ya maana kwako, yafanye kile kipindi ambacho akili yako imetulia, ukifanya maamuzi kwa haraka utajipoteza.
5. Usiende kulala ukiwa na hasira.
Unapolala huku una hasira, elewa kabisa hasira hizo utaamka nazo siku inayofuata, hivyo nenda kitandani ukiwa na amani itakusaidi sana.
Hizo ndizo tabia tano za msingi zenye uwezo wa kuboresha maisha yako ikiwa utaamua kuzifanyia kazi kwene maisha yako.
No comments:
Post a Comment