Taarifa zaidi Kuhusu Mtoto aliyetumbukizwa Chooni na Mama Yake Mzazi
Afya
ya mtoto Mwenge aliyenusurika kifo baada ya kutumbukizwa chooni na
kukaa humo kwa zaidi ya saa 14 kabla ya kuokolewa akiwa hai, inaendelea
kuimarika huku akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Kiomboi
Wilayani Iramba.
Mtoto
Mwenge alitupwa chooni na mama yake mzazi Winfrida Lori (23) mwanafunzi
katika Chuo cha Uuguzi cha Kiomboi Wilayani Iramba ambapo mama huyo
amekiri kujifungua mtoto huyo wa kiume katika Kijiji cha Luono Julai 3,
saa mbili usiku kisha kumfunga vitambaa mdomoni na kumtumbukiza chooni.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Kiomboi Regina Alex amesema afya ya Mtoto Mwenge
inaendelea kuimarika pamoja na hali ya mama mzazi wa mtoto huyo pia
inaimarika tofauti na hapo awali ambapo alikuwa dhaifu na kushindwa
kumnyonyesha mtoto.
“Winifrida
alikuwa hawezi kumyonyesha mtoto Mwenge hapo mwanzoni lakini sasa hivi
anamnyonyesha vizuri na maziwa yanatoka ya kutosha, Mtoto mwenge ana
hali nzuri na sasa amefikisha uzito wa kilogramu 2.9 hali ambayo
inaridhisha kwakweli”, ameeleza muuguzi huyo.
Muuguzi
Regina ameongeza kuwa licha ya mama wa mtoto Mwenge kuwa chini ya
ulinzi wa jeshi la polisi, ameendelea kumhudumia mtoto wake vizuri na
kwa upendo hali inayosababisha mtoto Mwenge kupata nafuu kwa uharaka.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amempa
jina mtoto huyo la Mwenge amesema kuwa jina hilo litamfutia mtoto huyo
majeraha ya kutupwa chooni na kuwa ishara ya kujiamini, kujipenda,
kujithamini na kumpa matumaini kama ambavyo mwenge wa huru umekuwa
ukifanya.
Dkt
Nchimbi amesema mwenge wa uhuru umekuwa ishara ya kuleta matumaini kwa
waliokata tamaa, upendo penye chuki na heshima penye dharau na hivyo
kitendo cha mama kumtupa mtoto ni kukosekana kwa amani, upendo na
heshima katika maisha ya mama huyo.
Ameongeza
kuwa anamtakia kila la heri mtoto Mwenge ili atakapokuwa alete heshima,
upendo na amani katika maisha yake na ya wazazi wake huku akifuta
kumbukumbu mbaya ya maisha yake wakati wa kuzaliwa.
Wakati
huo huo Dkt Nchimbi amewaasa wazazi na walezi kuwapa majina mazuri
watoto wao kwakuwa majina huwa ni sehemu muhimu ya maisha ya watoto wao
na hutafsiri maisha ya baadaye.
Dkt.
Nchimbi amesema jina linapaswa liwe na maono mazuri kwakuwa ndio hayo
yataambatana katika maisha yake lakini jina lenye baya huleta mambo
mabaya katika maisha ya mtoto.
No comments:
Post a Comment