STARTIMES YAWATAKA WATEJA KUWAHI OFA KEMKEM KWENYE BANDA LAO MAONESHO YA SABASABA
Kampuni
inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali
nchini, StarTimes, inawatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla
kutembelea banda lao kwenye maonyesho ya 41 ya Sabasaba yanayoendelea
jijini Dar es salaam.
StarTimes
inawapa wateja ving’amuzi vya bei rahisi vilivyounganishwa na
kifurushi cha bure kwa mwezi moja kwa shilingi 78,000 kwa dishi na
47000 kwa antena.
Pia
wateja wataweza kununua televisheni ya kidigitali kwa bei nafuu zaidi
na kupewa punguzo la asilimia 8% ambapo kutakuwa na inchi 40,32 na 24
yenye kingamuzi ndani yake na kukupa chaneli zaidi ya 100 za kitaifa na
kimataifa ili kufurahia ulimwengu wa kidigitali .
Mbali
na hayo,kutakuwa na bidhaa nyingine kama simu za kisasa na projekta
ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.
Lengo la kufanya hivi ni kumuwezesha kila mtanzania aweze kumudu gharama za matangazo na kufurahia ulimwengu wa kidigitali.
Pia
tungependa kuwahamasisha wateja wetu kulipia vifurushi tulivyonavyo ili
kuweza kutazama chaneli na vipindi vingi zaidi tulivyonavyo vya
kitaifa na kimataifa.
Hata
hivyo, wateja wa StarTimes wanafurahia matangazo ya moja kwa moja ya
kombe la mabara, Mwezi ujao tutaanza kuonyesha kombe la mabingwa
kimataifa (ICC), ligi kuu ya ujerumani (Bundersliga),ligi kuu Italia
(Serie A), ligi kuu Ufaransa (League 1) na mwakani kombe la dunia
litakalofanyika nchini Urusi.
Tunazo
tamthiliya, filamu za kiafrika na ulaya, kichina kihindi, vipindi vya
watoto na kadhalika.Vilevile utaweza kuangalia chaneli zaidi ya 37
mubashara na Bure kupitia APP yetu inayopatikana kupitia Google store,
App store au www.startimestv.com.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya StarTimes Pauline Kaka (katikati) na ofisa Huduma kwa
wateja Maria Mtoi (kulia) wakionesha moja ya bidhaa mpya iliyopo kwenye
banda lao leo.
Meneja
Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka akifafanua utendaji kazi wa
bidhaa zilizopo kwenye banda la kampuni hiyo kwa wateja waliofika
kujionea, kununua na kupata ofa zao.
Mfanyakazi
wa Kampuni ya StarTimes Pauline Kaka akimwandaliwa mteja TV ya Kisasa
baada kuinunua katika banda lao kwenye maonesho yanayoendelea ya 41
Sabasaba Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment