STAA OMMY DIMPOZ ALIKATA JINA LA SIMBA
Msanii wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz amekana madai ya kutaka kutumia jina la Simba na kusema majina ya wanyama yalimpitia mbali.
Kupitia
kipindi cha The Playlist cha Times FM, Ommy Dimpoz ameulizwa kwanini
katika moja ya picha alizopost Instagram akiwa na Mwana FA aliandika,
‘THIS IS SIMBA’.
Katika
majibu yake Ommy Dimpoz amesema, “no sikusema am Simba, THIS IS SIMBA
ni msemo unaotumika na mashabiki wa Simba Sport Club, kama umeona
Msemaji wetu Haji Manara anapendaga kutumia THIS IS SIMBA.
“Siku
ile tulikuwa tumetoka kwenye futari ya Simba tulikuwa tumealikwa, kwa
hiyo tulivyotoka tukapiga picha nilivyofika nikapost ile, kwa sababu
hiyo nikakumbusha tulitoka kwenye futari ya Simba na hata ukiangalia
mashabiki wengi wa Simba walikujua ku-comment,” amesema Ommy Dimpoz.
Muimbaji
huyo ameongeza kuwa huwezi kumuaminisha mtu kile unachoamini wewe na
hata ikitokea akahitaji kutumia jina la mnyama hatotumia la Simba kwa
sababu wanyama wapo wengi.
“Kiukweli
mimi majina ya wanyama yalinipitia mbali, kwa hiyo napenda kujiita hivi
hivi Ommy Dimpoz nimeridhika nalo, na hata nikiamua kujipa jina la
mnyama kuna wanyama wengi why nichague Simba, kuna Nyati kuna Swala,
kuna Kasuku yote hayo unaweza ukaamua kwa nini hufuate jina moja huo
utakuwa ukorofi,” amesisitiza.
Imekuwa
ni kawaida kwa wasanii wa Bongo Flava kujipa majina ya wanyama, Diamond
Platnumz anatumia jina la Simba, Dudu Baya anatumia jina la Mamba
ambalo kipindi cha nyuma lilileta mvutano kati yake na Shetta baada ya
kuanza kulitumia.
No comments:
Post a Comment