Sheria Mpya za Madini Mfupa mgumu kwa wawekezaji
Wakati Serikali ikiendelea kutafuta njia za kudhibiti kikamilifu rasilimali za nchi baada ya kupitisha sheria mpya ya maboresho ya Sheria ya Madini iliyopendekeza mambo kadhaa, wawekezaji katika sekta hiyo wameanza kutishika na kuanza kujiondoa.
Baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo, tayari mwekezaji mmoja kutoka Australia, Ian Middlemas kupitia kampuni yake ya Cradle Resources, amekosa dili la dola 55 milioni za Marekani (Sh121 bilioni) kupitia mradi wa uchimbaji wa madini ya niobium Panda Hill, uliopo nchini.
Kufuatia hatua hiyo, wataalamu kadhaa wa masuala ya uchumi wamesema ni lazima sheria hizo zitakuwa zimewashtua wawekezaji.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (Repoa), Dk Abel Kinyondo alisema watakimbia kwa muda mfupi tu.
Profesa Haji Semboja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kutaibuka baadhi ya kampuni ambazo zitafanya hivyo ili kutishia Serikali ili ichanganyikiwe na kubadilisha uamuzi wake.
No comments:
Post a Comment