Serikali yatangaza punguzo kubwa la bei kwenye dawa za tiba mbalimbali kwa binadamu
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara
zinazonunuliwa na kusambazwa Boahari ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa
asilimia 15 hadi 80 ukilinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD
kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama
alivyo agiza Rais Dk.John Magufuli.
Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari,
alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es
Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya
kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo
kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
No comments:
Post a Comment