Sababu za Wapenzi Wengi Kuchepuka
MPENZI msomaji wangu, kasi ya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa
ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa
kimapenzi unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa na hii ni kwa
sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao. Unaweza kuwa na
mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na
atakuwa na wewe katika shida na raha.
Lakini huyohuyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine.
Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wapenzi wanachepuka? Hicho ndicho
nilichopanga kukizungumzia leo. Yaani nitaainisha baadhi ya mambo
ambayo kwa uchunguzi wangu nimebaini ndiyo yanayochangia walio wengi
kuchepuka, wawe wako kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida.
TAMAA ZA KIMWILI NA PESA
Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia
kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine
hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na
kumhakikishia kwamba atampatia kila anachotaka, wanakubali mara moja
bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta
wanajenga mazoea. Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa
kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta
wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti.
Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke
bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa
na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.
na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.
TABIA ZISIZORIDHISHA Wapo ambao wanaishi maisha ya ajabu sana, yaani
wanaishi katika ndoa ama ndani ya uhusiano wakielekea kwenye kuoana
lakini hawaaminiani kabisa, kila mtu anakuwa na wasiwasi juu ya
mwenzake. Afadhali sasa iwe kutokuaminiana tu lakini wapenzi wanakuwa
hawasalitiani. Kuna wale ambao ni wazi hawatulii katika mahusiano yao,
yaani matendo yao tu yanaonesha dhahiri kwamba, uaminifu ni sifuri. Kuwa
karibu sana na watu wa jinsia tofauti na kuwa na mawasiliano nao ya
siri au mwanamke anapomuwekea mumewe vikwazo katika tendo la ndoa
anatarajia akafanye na nani kama siyo kumwambia akatafute wengine nje?
Ndiyo maana wanaowanyima unyumba waume zao hata wanaposikia kwamba
wanasalitiwa wanakuwa hawana nguvu ya kuwashutumu wapenzi wao,
utamshutumuje wakati wewe humtimizii katika mambo flani? Si hivyo tu,
kwa wanaume nao wengine wamekuwa wakiwasusa wake zao na kukaa siku mbili
ama zaidi bila kuonekana nyumbani ama kama atarudi basi usiku wa manane
akiwa amelewa na hana mpango kabisa na mke wake. Katika mazingira hayo
unadhani nini kinaweza kutokea kama siyo mwanamke kutafuta mwanaume
atakayempatia mapenzi?
KUWEPO KWA MAPENZI YA KILAGHAI
Tunapozungumzia mapenzi tunaweza kuyagawanya katika makundi mawili,
mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Walio katika mapenzi ya kweli
huwezi kuwasikia wamesalitiana. Ila wale walio katika mapenzi ya
kudanganyana kusalitiana ni kitu cha kawaida kwao hivyo kujikuta kila
siku wakifumaniana.
UDHAIFU KWA WAPENZI Udhaifu ambao umezungumziwa hapa ni wa kimaumbile
ambao hata hivyo wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kwamba,
haiwezi kuchukuliwa kama sababu ya kumsaliti mpenzi wako uliyempenda kwa
dhati. Kwa mfano, mwanaume unakuwa ‘Functionless’ yaani jogoo hawiki
(tatizo ambalo si la kujitakia) na mke wake hayuko tayari kuendelea kuwa
naye hivyo kulazimika kuomba talaka. Lakini mwanaume anakuwa mgumu wa
kutoa talaka kutokana na jinsi anavyompenda.
Wengi wao wanachokifanya ni kuendelea kuwa katika ndoa huku
wakiangalia uwezekano wa kuwa na uhusiano na mtu mwingine wa nje. Kwa
wanawake nao yawezekana mwanamke hazai (tatizo ambalo si la kujitakia
pia) na mwanaume anahitaji mtoto, atakachokifanya ni kutoka nje kwa siri
lakini pia inaweza kufikia hatua mwanamke akagundua. Kwa kifupi ni
kwamba kusalitiana kwa wanandoa kumekuwa kukitokea kutokana na kuwepo
kwa mazingira fulani ambayo baadhi yao wamekuwa wakishindwa kujizuia
nayo na hivyo kujikuta wanatoka nje ya mahusiano.
Ila sasa nalazimika kwa nguvu zote kuwashauri wale walio katika
uhusiano wa kimapenzi, namaanisha wapenzi wa kawaida, wachumba ama
wanandoa, tusiwe na tamaa za kijinga na kufikia hatua ya kuwasaliti
wapenzi wetu. Hivi unajisikiaje unapomvulia nguo mtu ambaye wala hana
‘future’ na wewe? Hivi na wewe ukifanyiwa hivyo na mpenzi wako
utajisikiaje? Elewa maumivu utakayoyapata pale utakaposikia mpenzi wako
ana uhusiano na fulani ni hayohayo atakayoyasikia mwenza wako. Kuwa
muaminifu, ridhika na unachokipata kwake, muoneshe mapenzi ya dhati naye
atafanya hivyohivyo na kujikuta mnayafurahia maisha yenu.
No comments:
Post a Comment