Rais Magufuli: Mtoto wa Mdogo wangu alipewa Mimba akiwa Mwanafunzi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema
anapenda taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundation na si
zinazohamasisha wanafunzi wazae kisha warudi shule.
Rais
Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50
za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
“Nazipenda
taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundationa na si zinazotaka
watu wazae halafu warudi shuleni. Mmekalia kusema kuwa watu wazae halafu
warudi shule, sasa si watazaa kila mahali,” alihoji Rais Magufuli.
“Hata
kwangu kuna watu wanaozaa na wala hawajabakwa, hata mtoto wa mdogo
wangu alizaa bila kubakwa, alipoulizwa imekuwaje akajibu kwa kisukuma
alafu akanizalia mtoto akamuita John, akakaa kidogo akazaa tena mtoto
mwingine akamwita Samia,” alisema Rais Magufuli huku watu wakicheka.
No comments:
Post a Comment