Rais Magufuli Atoa ONYO Kwa Wanasiasa Waropokaji.......Awataka Polisi Wafanye Kazi Bila Kumuogopa Mtu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ametoa onyo
kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa
nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema
kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara
yake.
"Niwaombe
wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu
wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule
Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini
usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.Msitufanye tukafika huko"
"Kwanini
hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule.
Lakini kwa kutaka sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako
ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule...nataka polisi mfanye
kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na
mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie
polisi akiwa kule ndani," amesema Rais John Magufuli na kuongeza;
"Juzi
mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao
walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni
mwa walioagiza hizo uniform za jeshi.
"Endeleeni
kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia...
mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini
ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani
"Kuna
vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani,
tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala
hawajasaini mkataba wowote.
"Hamkuuliza
vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si
watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu?
"Sijui
haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili
Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu."
No comments:
Post a Comment