RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI
RAIS
Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha
kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa
tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya
kuishi kinyume cha taratibu.
Kauli
hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao
hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.
Amesema
haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya
kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji
tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila
ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu
Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”
Waziri
Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni
kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo
nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa
hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”
Amesema
Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji
raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na
uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.
"Hawa
Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini
wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli
ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani
kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."
Pia
Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji
hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. "
Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri
ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika
ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."
Hata
hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchungilzi wa kina ufanyike kwa watu wote
walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi
matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments:
Post a Comment