Trending News>>

Okwi Ala Shavu Ligi Ya Uganda



Mshambuliaji mpya wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda.
STRAIKA mpya wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, ameng’ara nchini kwao baada ya kutajwa kwenye kikosi bora cha msimu wa Ligi Kuu ya Uganda iliyomaliza hivi karibuni.
Okwi ambaye alikuwa akiichezea SC Villa ya nyumbani kwao kabla ya hivi karibuni hajasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba, aliitumikia timu hiyo kwenye mechi 13 za Ligi Kuu ya Uganda na kufunga mabao 10.
Mganda huyo aliyekuwa na kikosi cha Klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark kabla ya kusaini mkataba wa miezi sita na SC Villa, ametajwa kwenye kikosi hicho katika Tuzo za Ligi Kuu ya Uganda zilizofanyika usiku wa juzi Jumatano nchini humo.
Kikosi kizima cha wachezaji bora wa ligi hiyo kipo hivi; Isma Watenga (Vipers), Nico Wadada (Vipers), Halid Lwaliwa (Vipers), Habib Kavuma (KCCA FC), Timothy Awany (KCCA FC), Saddam Juma (Express FC), Mutyaba Muzamir (KCCA FC), Tadeo Lwanga (SC Villa), Muhammad Shaban (Onduparaka), Emmanuel Okwi (SC Villa) na Geoffrey Sserunkuma (KCCA FC).

No comments:

Powered by Blogger.