Trending News>>

Okwi akabidhiwa mjengo Sinza

UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar, umempatia nyumba mshambuliaji wake, Em­manuel Okwi, maeneo ya Sinza kwa ajili ya makazi akiwa anaitumikia timu hiyo. Okwi amesaini Simba hivi karibuni kwa mkataba wa mia­ka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, bosi kutoka Simba ameeleza kuwa, tayari uongozi huo umeshampatia nyumba ya kuishi Okwi maeneo ya Sinza am­bapo atakuwa akiishi pamoja na wachezaji wenzake wa kimataifa.

“Simba ina utaratibu kuwa kila mchezaji atakayewasili nchini lazima wampatie ny­umba ya kuishi, hivyo Okwi atakwenda kuishi Sinza pamo­ja na wachezaji wengine kati­ka nyumba iliyoandaliwa kwa ajili yao.

“Hata hivyo nyumba hiyo watakaa kwa muda hadi pale ujenzi wa kiwanja chetu utakapokamilika ambapo timu italazimika kuhamia Bunju kwa ajili ya ukaribu wa kiwanja cha kufanyia mazoe­zi,” alisema bosi huyo.
Alimalizia kwa kusema kuwa, nyumba zote am­bazo zimewekwa kwa ajili ya wachezaji, zina ubora kwa ajili ya kumfanya mchezaji ajisikie vizuri.

No comments:

Powered by Blogger.