Trending News>>

Mwanamke mwenye ulemavu wa miguu abakwa Zanzibar


Jamii ya watu wa Zanzibar yaombwa kukaa karibu na watu wenye ulemavu kwani vijana hufanya mambo kama wanyama.
Maneno hayo yemesemwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Unguja kamishna msaidizi wa Polisi Juma saidi Khamis baada ya kijana Ame Mwadini Nahoda mwenye umri wa miaka 19 mkaazi wa Kichaka Mabundi Mwera shehia ya ubago amembaka msichama wa miaka 20 ambae ni mlemavu wa miguu na pia ni bubu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda Juma Saidi Khamis amesema tukio hilo la kusikitisha limetoke Jully 12, 2017 majira ya saa tano asubuhi na kuripotiwa kituo cha polisi dunga.
“Kumbaka mwanamke ambae ni mlemavu nikosa kubwa kisheria na mpaka sasa mtuhumiwa tumesha mkamata na tunakamilisha taratibu za upepelezi ili jalada tulipeleke kwa mkurugenzi wa mashta kwa ajili ya hatu za mahakamani” alisema msaidizi wa kamishna wa Polisi Juma.
Nae Mratibu wa wanawake na watoto katika shehia ya Ubago Mwajuma Hassan Abdallah imeomba jamii kuto ficha vitendo hivyo ili sheria ziweze kuchukuliwa.
Mtuhumiwa watukio tukio hilo anatarajiwa kufikishwa mahakamani pale tu upelelezi utakapo kamilika.

No comments:

Powered by Blogger.