Trending News>>

Mkhitaryan atoka kitambi, United wamfuta

Mambo mengi yanaendelea hivi sasa lakini kubwa mojawapo ni kwamba baada ya bata refu la likizo sasa wachezajj wa Ulata wanarudi vilabuni mwao kuanza maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Wachezaji wa Manchester United nao wameanza kurudi kujianda na safari ya kwenda Marekani na timu yao na waliorudi tayari walifanyiwa hadi photoshoot ya jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Henrikh Mkhitaryan ni mmoja kati ya waliorudi na ukifungua ukurasa wa Instagram wa Manchester United naye utaona ni kati ya wachezaji waliopiga picha wakiwa na jezi mpya ya klabu hiyo.
Lakini usichokijua ni kwamba kuna picha ya Mkhitaryan ambayo nayo ilipaswa kutangaza jezi hizo lakini imeondolewa katika orodha ya picha ambazo zitatumika kutangaza uzi huo mpya wa United.
Picha hiyo mwanzo United waliipost katika kurasa zao na ikaondolewa kwa sababu ya muonekano wa Mualmernia huyo ambaye anaonekana wazi alikula bata la kupitiliza wakati wa likizo.
Mkhitaryan anaonekana kuanza kutoka kitambi na kunenepa suala ambalo United wameona sio vyema kulionesha sana, na ili kulinda image ya mchezaji huyo ndio maana Manchester wakaamua kuiondoa picha hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.