Mke Wa Mtu Anusurika Kichapo Mwanza Kisa Mtoto Mwenye Baba Watatu Vidume Vyakutana Live!
Ama kweli ule usemi wa siku za mwizi arobaini
unatokea katika mazingira usiyoyategemea!! Mwanamke mmoja ambaye ni mke
wa mtu mkazi wa Igoma jijini Mwanza amenusrika kutembezewa kichapo na
kuwaacha watu midomo wazi baada ya kubainika kuwa mtoto mwenye umri wa
mwaka mmoja aliyekuwa anaishi naye kwa mume wake ana baba watatu.
Mwanamke huyo amenusurika kipigo leo asubuhi baada ya
kushindwa kubainisha ukweli juu ya uhalali wa mtoto kutoka kwa wanaume
wawili aliokuwa anawavuna pesa huku mme anayeishi naye akishangaa kuona
misaada mbalimbali wanayopata watoto anaoishi nao kwa madai kuwa
wanahudumiwa na wajomba zake.
Inaelezwa kuwa mwanamke huyo anayeishi na mume wake,huku
mume wake akiamini kuwa yeye ndiyo baba wa mtoto kati ya watoto wawili
anaoishi nao,kumbe mambo ni tofauti kabisa kwani mtoto huyo analelewa na
baba wengine wawili na yeye ni wa tatu.
Wanaume hao watatu wanaishi jijini Mwanza,mmoja
Igoma,mwingine mfanyabiashara wa Chips katika Chuo Kikuu cha Sauti
Mwanza na mwingine anaishi Igogo.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mwanamke huyo
alikuwa anawaambia wanaume hao kila mmoja kwa wakati wake kuwa amezaa
naye na hivyo kuhudumia mtoto huyo.
“Huyu mama anaishi na mme wake,alikuwa anamuaga mmewe
kuwa anaenda kwa mjomba wake,anaweza kukaa hata wiki moja na anarudi na
nguo za mtoto anamwambia mmewe kuwa zimenunuliwa na wajomba zake kumbe
zimenunuliwa na mwanaume mwingine”,walieleza mashuhuda wa tukio hilo.
“Anaporudi nyumbani kwa mmewe,huwa hapokei simu za hiyo
michepuko mingine huwaambia wasipige simu kuwa anaishi nyumbani wazazi
wake hawapendi kumuona anaongea na simu,kumbe yupo kwa
mumewe”,waliongeza.
“Kilichotokea leo ni kwamba kaenda kwa mwanamme mwingine
mmoja kati ya hao michepuko wake,simu ikawa inaita imeandikwa ‘Baba
Watoto’ akawa hapokei,kila ikiita anaikata,baadae akaenda kuoga,ndipo
mchepuko ukaamua kuanza kupekua simu kuangalia hiyo namba ni ya nani
haswa”,waliisimulia
Hata hivyo inaelezwa kuwa mwanamme huyo baada ya kupekua
simu hiyo alibaini kuwa kuna wanaume zaidi ya mmoja wanahudumia mtoto
huyo ndipo akahamaki na kuanza kuwapigia simu mmoja baada ya mwingine
ili kujua ukweli.
“Kutokana na sintofahamu hiyo wanaume wote watatu
akiwemo anayeishi na mwanamke huyo wakakutana na ndipo vurugu ikaanza
wakitaka kumpiga mwanamke huyo lakini wananchi waliokuwa eneo la tukio
wakamnusuru asipigwe”,walieleza mashuhuda wa tukio hilo.
Wanaume wawili “Michepuko” waliamua kumuomba mwanamme
anayeishi na mwanamke huyo aende na mke wake huku mwenye mke akidai
lazima akapime DNA ili kubaini kama watoto wote anaoishi nao ni wa kwake
au la!.
Wakizungumza eneo la tukio baadhi ya wananchi walisikika
wakisema mwanamke huyo ni miongoni mwa wanawake wengi ambao wamekosa
uaminifu na kuwa na tamaa ya pesa ndiyo maana siyo kitu cha ajabu kuona
mwanamke ana wanaume zaidi ya mmoja na wote hawajuani.
No comments:
Post a Comment