MGANGA WA JADI AUAWA NAMTEJA WAKE BAADA YA KUSHINDWA KIMTIBU!
Mganga wa jadi, Revocatus Kanjalanga (65) katika Wilaya ya Nkasi mkoani
Ruvuma ameuawa kikatili kwa kuchomwa na mkuki mgongoni na mtu
asiyefahamika ambaye anadaiwa kuwa ni mteja wake wa muda mrefu.
Ilielezwa kuwa wateja wa mganga huyo walikuwa wakimlalamika kuwa kwa
kipindi kirefu mganga huyo amekuwa akiwatibu kwa kuwatoza fedha nyingi
za malipo ya matibabu lakini wamekuwa hawaponi kupitia uganga wake.
Mtoto wa mganga huyo aliwaambia waandishi kuwa baba yake aliuawa juzi
saa 1:30 asubuhi kwa kupigwa mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani
katika kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani
Nkasi.
Alisema kuwa kwa muda mrefu watu ambao walikuwa wanatibiwa na baba yake
walikuwa wakilalamika kutozwa fedha nyingi pamoja na mifugo lakini
hawaponi, hali iliyosababisha kuanza kumuona kama tapeli.
Alisema watu hao walikuwa wanalalamikia kutofanikiwa matatizo yao ya kiafya, kutafuta mali pamoja na mazindiko.
“Pengine malalamiko hayo ndiyo yaliyosababisha mtuhumiwa aamue kumuua
kwa kumchoma mkuki mgongoni, na aliyefanya hilo hajapatikana na mpaka
sasa anatafutwa,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anasakwa.
No comments:
Post a Comment