Trending News>>

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Nimebahatika kutembelewa na mkwe wangu wiki kadhaa sasa, nilifurahi nikashukuru kwa kupata ugeni mzito ukizingatia kwamba nakaa na shemeji zangu hapa, mmoja anatafuta kazi mwingine yupo chuo anakaa hostel ila huwa anarudi hasa weekend.
Tabia ambazo amenionyesha na hakika niseme wazi tu kua zinanikera na kuukwaza moyo wangu na Mara hii naanza kujihisi unyonge sana ndani ya nyumba yangu
huyu mwenzangu alizaaga mtoto kipindi cha nyuma huko katika pita pita za ujana na huyu mtoto yupo kwa mama yake na anasoma boarding school na kila kitu kinalipiwa na baba yake hapa nami wala sina tatizo na hilo, sasa tangu mama mkwe aje akikaa na mwanae hadithi ni kumzungumzia huyo mama wa mtoto wee na kibaya zaidi anasema wazi kabisaa kua huwa anakwenda kumuona na kukaa hapo kwake yaani kwao na mumeo wangu, yaani anamsifu kabisaa kuwa anasaidia sana na anamshukuru.
Mbaya zaidi baba watoto baada ya ajali mbaya aliyoipata na kupata tatizo la nyonga yupo tu haendi kazini zaidi zaidi akitoka huwa anakwenda dukani kwetu kusaidia biashara, mimi hutoka asubuhi kwenda job na kurudi jioni na kutokana na heka heka za foleni najikuta Mara nyingine nachelewa kufika nyumbani mpaka saa 12 ndio naingia ila kawaida yangu ni ile ile kua chakula cha jioni napika mwenyewe hata Dada wa kazi hapa anafahamu hilo, mama mkwe nikichelewa hiyo kurudi anaanza maneno kua “sasa watakula saa ngapi? Mwanae si atachelewa kunywa dawa? Kwa namna hii atapona kweli?” Yaani ni maneno juu ya maneno yeye anamfikiria mwanae mtu mzima hawa wajukuu walio wadogo hawaoni? Nifanyeje sasa? Niache kazi ili nimuhudumie mwanae ale saa 12 jioni badala ya saa 2 usiku au?
Nimekosa uhuru na hamu ya mume wangu kwa kweli maana hata chakula kiwapo mezani nikimpakulia mwanae anakadiria kwa kuuliza “mbona kidogo sana? Atashiba kweli?” Inamaana mimi nampunja mwanae!? Mimi niliyekaa nae miaka yote hii na watoto wote hawa nimpunje mwanae chakula lol!? Mama mkwe nakupenda sana, sana sana mamangu ila Tafadhali bila kusubiri siku nitakayoteleza na kufungua kunywa changu Leo nitamwambia mwanao bora uende.
Shukrani zote anastahili Allah (subhanahu wata’ala) mola wa viumbe vyote, Rehma na Amani. Mwanzo kabisa naomba nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote waliochangia Mawazo yao katika Uzi wangu, mimi ni binaadamu kwa namna moja ama nyingine naweza kua namkosea yeyote ila nnachoweza kusema “Tupendane kwa ajili ya Allah ” maana sisi sote si wakamilifu.
Pili naomba nitoe ufafanuzi mdogo tu kwa faida yetu mimi simnyanyasi mume wangu kama wengine wanavyosema, niliposema yupo tu nyumbani sikumaanisha kua hana kazi kazi anayo ila kama kawaida masahibu kaumbiwa binadamu by February mwaka huu alipatwa na ajali ambayo imemlazimu kupewa likizo ya ugonjwa lakini pia sina chuki na ndugu wa mume mpaka mama mkwe wangu, kwa maana shemeji zangu wako hapa tangu walipomaliza kipato cha nne mpaka Leo hii mmoja wao kamaliza chuo kikuu Mlimani na mwingine yupo Bandari College-Tandika, nipo nao hapa na kama ningelikua siwapendi basi wasingeweza kuishi hapa ili wakafikia malengo yao.
Usiku ule ulikwenda vizuri, shukrani kwake M/Mungu kutokana na miaka 7 tuliyoishi moja ya bahati kubwa niliyojaaliwa ni mume wangu kuelewa situation niliyonayo kwa wakati husika kwa kupitia uso wangu, kabla ya hata kueleza ya moyoni mwangu kwa undani alinikatisha na kunieleza hata yeye hafurahii ila hana jinsi alichoniambia “Mvumilie mama yangu ndio mapungufu yake, umeweza kuyavumilia ya kwangu naomba na ya kwake uyabebe” nami nimekubali kuyabeba na kwa uweza wa Allah sitayashusha mpaka pale M/Mungu atakapoamua kunitua.
AZIMIO TULILOFIKIA: Ni yeye kwenda kushinda dukani kwetu mpaka saa 3-4 usiku mdogo wake anapofunga duka kisha warudi wote, Leo itakua siku ya 3 kutekeleza hili, Alhamdullilah mambo yanakwenda vizuri na naimani yatakua vizuri zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.