Kwa nini Diski Kuu ktk Kompyuta za Windows huitwa Drive ‘C’ na si A au B?
Kama ni mtumiaji wa kompyuta zinazotumia Windows utagundua ya kwamba
mara zote diski uhifadhi kuu (hard drive) katika kompyuta yako hupewa
jina la Drive C.
Ukiwa unapakua (install) programu ya Windows kwenye kompyuta yako hakuna
kabisa uwezo wa kuipa jina la A wala B, na diski zingine
utakazochomeka n.k huchukua herufi nyinginezo lakini kamwe si A wala B.
Sababu – Kihistoria…
Kabla ya teknlojia za ‘hard disk’ kuja kompyuta miaka ya zamani zilikuwa zinakuja na Floppy Disk.
Muonekano wa kompyuta ya zamani, ikiwa ina maeneo mawili kwa ajili ya Floppy Diski
Eneo moja, A: lilitumika kuweka Floppy Drive ambayo ndio ilikuwa na
programu endeshaji (OS) ya kompyuta na wakati mwingine nafasi ya pili
kwa wenye uwezo mkubwa wa pesa basi walikuwa wanatumia kusomea floppy
diski ya pili; hii ilihusisha kutumia programu mbalimbali na kadhalika.
Na hiyo historia ya Drive A na B. Ni kutokana na hivi ndio basi ata pale
ambapo teknolojia ya harddisk, ujazo mkubwa zaidi ulipokuja ukapewa
eneo la Drive C.
Drive D huchukuliwa na mfumo wa kusoma CD/DVD.
Muonekano wa floppy diski ikiwa imechomekwa kwa kutumia ‘adaptor’ ya kisasa kwa ajili ya kusomea Floppy Diski
Je ni muhimu sana hali kuendelea hivi?
Ndio, kulazimisha diski yenye programu endeshaji ya Windows kuwa A
kunaweza leta ugumu mkubwa kwa kompyuta hiyo kuweza kufanyakazi bila
matatizo.
Mfumo mzima wa Windows wa sasa umejengwa katika kuelewa ya kwamba
programu endeshaji hiyo huwa inakaa kwenye Drive C, waliojaribu kuweka
kwenye A au B kiulazima wamejikuta wakipata tabu.
Inasemekana kutokana na kufahamu ya kwamba teknolojia za uhifadhi data
za floppy diski kuwa za kizamani basi ata kompyuta na programu endeshaji
huwa zinasoma disk A au B kwa uangalifu sana kama zimechomekwa. Hii ni
kutokana na kwamba teknolojia hizo za kizamani zina ubora mdogo na hivyo
zinaweza ruhusu virusi kushambulia kompyuta kwa urahisi zaidi.
Muonekano wa Floppy Diski za ukubwa mbalimbali, ya kwanza kushoto
ilikuwa inatumika baadhi ya sehemu tuu (makampuni n.k). Ya katikati na
kulia ndio zilikuwa zinatumika zaidi.
Je wewe ulitumia kompyuta kipindi ambacho Floppy Diski zilikuwa bado kwenye utumiaji sana au ndio umefahamu kuhusu uwepo wake?
Chanzo: Superuser.com na vyanzo mbalimbali
Tazama video Mtoto amvua kofia
Papa Francis
Papa Francis
No comments:
Post a Comment