Trending News>>

JIFUNZE KITU



Kuna mdada alikutana na mkaka wakati wako safarini. Yule kaka akamuomba mdada namba ya simu. Njiani akamnunulia kila kitu alichotaka, alipofka standi mkaka akamlipia usafiri mpaka nyumbani kwao.

Basi wakawa wanawasiliana kila siku. Siku nyingine anamuita wanatoka wanakula na kunywa na hela anampa.

Yule dada akawaambia marafiki zake nimepata bonge la bwana jamani, nitake nini mimi nisipewe??? Mashoga wakamwambia weeee ebu jaribu..?! Yule dada akampigia yule jamaa akamwambia leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saloon nimemis sana kwenda club na marafiki zangu. Yule jamaa akamwambia ok akamtumia laki 3 ya saloon na kumwambia kama isipomtosha aseme.
Wenzie wakasema “lol shoga bwana umempata“. Ilipofika jion yula mwanaume akapiga simu kwa yule binti akamuuliza club gani mnakwenda??? Yule dada akataja club wanayotaka kwenda, yule bwana akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue me mtanikuta huko.

Baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake, walipofika wakanywa, wakala na kucheza. Wakarudishwa homu kama walivyoahidiwa. Siku ya pili yule bwana akamwambia yule dada nataka kuzungumza na wewe ila tafadhali njoo peke yako. Yule dada akajikoki akaenda alipofika kule yule kaka akamwambia nimempenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe naomba ukamwambie hisia zangu hizi wala sina plan ya kumchezea nitamuoa kabisa..! Sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndie anaestahili kupajua nyumbani kwangu.

Yule dada akamwambia mimi je??? Yule kaka akamuuliza wewe nini?? Yule dada akamjibu mimi utanipeleka wapi kwa hiyo..? mimi ndio unaniacha? Yule kaka akamwambia mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi, nilikuchukulia kama rafiki ndio maana sijawahi kuzungumza na wewe suala la mapenzi. Mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo. Tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele. Kam kuna kitu nimekifanya kwako ni kukushika mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya.
Dada huku akilia akamwambia mbona ulikua unanihonga???Yule kaka akacheka akasema “sikuwahi kukuhonga, mimi nilikua nakupa”.

No comments:

Powered by Blogger.