Habari nyingine kubwa zilizoripotiwa kwenye Taarifa ya Habari usiku huu
Habari ya Clouds TV – Norway kuboresha uhusiano na Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje ya Norway Borge Brende amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Norway itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania hasa kwa kuboresha huduma za kijamii na uwekezaji katika miradi mikubwa ya maendeleo.
“Uhusiano wa Tanzania na Norway umedumu kwa miaka 55 na tumeshirikiana katika mambo mengi yakiwemo kuendeleza elimu na miundombinu mbalimbali. Sasa tunatarajia kushirikiana zaidi na Tanzania kwa kuwekeza katika miradi mikubwa kama vile uzalishaji wa umeme, kuchakata gesi na kuzalisha mbolea.” – Borge Brende.
Habari ya Chanel 10 – Dawa za Serikali zimekutwa katika Maabara bubu Songwe
Wakati Serikali ikipinga uuzaji wa dawa za binadamu kiholela hali ni tofauti katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambako kumegundulika Maabara bubu ikiwa na vifaatiba kinyume na utaratibu. Ugunduzi huo umekuja baada ya raia wema kutoa taarifa kwa Halmashauri ya Mbozi na Mganga Mkuu Aneth Makaye alifanya ziara ya kushtukiza lakini mmiliki wa Maabara hiyo alitokomea kusikojulikana.
“Tunaenda pale Zahanati za Serikali tunatibiwa, tunapoomba dawa tunaambiwa hakuna lakini leo hii unakuta Maabara za vichochoroni zimekutwa na dawa za Serikali. Sasa je, tujiulize wananchi ni kwamba ina maana hao wenye Maabara za vichochoroni wana ubia na Serikali? Kwa nini dawa za Serikali zikutwe huku?” – Ayub Mihambo (Mwananchi Mlowo)
“Hichi kituo kinaendesha huduma ambayo hakijaruhusiwa. Mfano, hiki ni kwa ajili ya upimaji wa Malaria lakini ni mali ya Serikali vinatakiwa kuwepo kwenye vituo vya Serikali sio kwao. Sasa unashangaa zinafikaje huku, watu wanalalamika dawa hakuna lakini dawa zipo wanauziwa. Watatuambia wao wanazipata wapi zinakuwa kwenye vituo vyao na vituo vyetu vinakosa dawa.” – Aneth Makaye.
Habari ya Clouds TV – Norway kuboresha uhusiano na Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje ya Norway Borge Brende amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Norway itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania hasa kwa kuboresha huduma za kijamii na uwekezaji katika miradi mikubwa ya maendeleo.
“Uhusiano wa Tanzania na Norway umedumu kwa miaka 55 na tumeshirikiana katika mambo mengi yakiwemo kuendeleza elimu na miundombinu mbalimbali. Sasa tunatarajia kushirikiana zaidi na Tanzania kwa kuwekeza katika miradi mikubwa kama vile uzalishaji wa umeme, kuchakata gesi na kuzalisha mbolea.” – Borge Brende.
Habari ya Chanel 10 – Dawa wa Serikali zimekutwa katika Maabara bubu Songwe
Wakati Serikali ikipinga uuzaji wa dawa za binadamu kiholela hali ni tofauti katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambako kumegundulika Maabara bubu ikiwa na vifaatiba kinyume na utaratibu. Ugunduzi huo umekuja baada ya raia wema kutoa taarifa kwa Halmashauri ya Mbozi na Mganga Mkuu Aneth Makaye alifanya ziara ya kushtukiza lakini mmiliki wa Maabara hiyo alitokomea kusikojulikana.
“Tunaenda pale Zahanati za Serikali tunatibiwa, tunapoomba dawa tunaambiwa hakuna lakini leo hii unakuta Maabara za vichochoroni zimekutwa na dawa za Serikali. Sasa je, tujiulize wananchi ni kwamba ina maana hao wenye Maabara za vichochoroni wana ubia na Serikali? Kwa nini dawa za Serikali zikutwe huku?” – Ayub Mihambo (Mwananchi Mlowo)
“Hichi kituo kinaendesha huduma ambayo hakijaruhusiwa. Mfano, hiki ni kwa ajili ya upimaji wa Malaria lakini ni mali ya Serikali vinatakiwa kuwepo kwenye vituo vya Serikali sio kwao. Sasa unashangaa zinafikaje huku, watu wanalalamika dawa hakuna lakini dawa zipo wanauziwa. Watatuambia wao wanazipata wapi zinakuwa kwenye vituo vyao na vituo vyetu vinakosa dawa.” – Aneth Makaye.
No comments:
Post a Comment