Diamond Kampeleka Zari Mombasa na Kuwachamba Wanaomsema Vibaya
Pia amewajibu wanaotaka mpenzi wake abaki akiwa mnyonge baada ya kupata matatizo ya kufiwa na mama yake mzazi wiki chache zilizopita.
“Kuna
vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu….
Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem
tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna
mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila
mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni
na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya
kwanza 😛.” ameandika Diamond Instagram.
Diamond
amefikia hatua hiyo baada ya watu kumponda mpenzi wake Zari The Boss
Lady, ambaye siku ya jana alikuwa Instalive na mkali huyo wa Eneka
wakijiachi kimahaba, hali iliyofanya mitandao ya kijamii kumponda kuwa
anaonyesha hana uchungu wa kufiwa na mzazi wake, kazi yake ni
kujiendekeza na mapenzi.
1 comment:
Yap you made it...
Post a Comment