Bradley atuachia funzo hili wanamichezo...
Kifo cha Bradley Lowery kimeugusa ulimwengu mzima wa soka na
kila mtu anamuongelea Lowery kwa majonzi makubwa, na hakika wengi
tumesikitishwa na msiba wa mtoto huyu.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika habari zake na jinsi alivyokuwa anapambania uhai wake ni story ambayo ilikuwa inaumiza sana na kusikitisha sana.
Lakini kupitia Lowery tufahamu kwamba michezo ni sehemu moja ya maisha na maisha yetu yako ndani ya soka na soka hili linaweza kutufanya tuyafurahir maisha.
Pamoja na ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua Bradley lakini sehemu pekee ilipokuwa faraja yake ilikuwa ni nyasi na majukwaa ya Stadium Of Light uwanja wa Sunderland.
Tujifunze matatizo ni ya kila mmoja wetu na tumeumbiwa sisi lakini hilo lisituzuie kufanya kile ambacho kinafariji mioyo yetu na hii itatusaidia kufurahi na kuongeza siku za kuishi.
Soka likitumika vizuri inaweza kuwa faraja kwa waliopoteza faraja,likawa uhai kwa wanaokaribia uhai na soka likawapa nguvu waliochoka kama Defoe na Sunderland walivyofanya kwa Bradley.
Tupendaneni na tufarijianeni wakati wa matatizo, soka linatuunganisha sana na michezo inatufanya tuwe ndugu, kwa jinsi Defoe alivyomjali mshabiki wake akawa kama ndugu na sisi vivyo hivyo.
Mwisho kabisa maisha haya ni mafupi sana na kila mtu atakufa, ni vyema tuitumie vyema kila pumzi tunayopewa kwa kufanya mambo mema na yenye kutupa furaha katika maisha yetu.R.I.P BRADLEY LOWERY.

No comments:
Post a Comment