Trending News>>

Young Killer akubali yaishe


Yale majibizano kati ya Nay pamoja na Msodoki yameendelea tena, baada ya Nay wa Mitego kusema amesikia ngoma ya Young Killer lakini kwake ni kama jingo kwani wimbo huo haujamilika. Msodoki amekiri 'True Boya' si wimbo rasmi kwani hakufanya serious.

Rapa Young Killer
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Young Killer amesema wimbo wake huo ambao aliutoa rasmi kwa ajili ya kumjibu Nay wa Mitego amekiri si wimbo rasmi kwake ndiyo maana hakuwa serious sana katika ngoma hiyo na kusema wimbo wake rasmi unakuja muda si mrefu.
"Kwanza mimi sijafanya serious wimbo wangu 'True Boya' kwa sababu sijauandaa kwa muda mrefu sana ni wimbo nilioundika kwa masaa mawili tu nikaingia studio nikarekodi ndiyo maana kimekuwa ni ki verse kimoja tu, kwa hiyo siyo wimbo wangu rasmi lakini ni wimbo ambao nahitaji upigwe na uendelee kusikika kwa sababu ni wimbo ambao unakila sifa ya kusikilizika na kupendwa kwa kila kile nilichokifanya japo sikuwa 'serious' " alisema Young Killer 
Mbali na hilo Young Killer amedai kuwa wimbo wake rasmi ambao amefanya na msanii Harmonize utatoka baada ya wiki mbili kutoka sasa na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kusikiliza ngoma hiyo ambayo mwenyewe anaamini kuwa italeta shida mtaani.

Nay wa Mitego aliingia katika majibizano ya maneno na Young Killer baada ya rapa huyo kuachia wimbo wake mpya wa 'Moto' ambao ndani yake alimchana Young Killer kwa kumuambia kuwa anakaribia kurudi kwao Mwanza baada ya kazi ya muziki kuonekana kumshinda, kwa kile anachodai kuwa rapa huyo aliwakosea sana watu ambao walifanikisha yeye kuwa msanii mkubwa, hivyo alimtaka kuwa na nidhamu ikiwezekana kuwaomba msamaha watu hao ili wakunjue roho kwake.

No comments:

Powered by Blogger.