Weusi tumeacha ushamba : Joh Makini
Rapa kutoka Weusi Kampuni, Joh Makini
amefunguka kuwa kampuni yao kwa sasa haina ushamba tena kwenye muziki
kwa kuamini kuwa video ndiyo inaweza kukuza muziki wao na kuwapeleka
sehemu kubwa zaidi.
Wasanii kutoka Weusi, Kushoto ni G Nako, katikati ni Joh Makini na kulia ni Nikki wa Pili
Akizungumza
na eNewz Joh Makini, amesema kuwa anacho amini kwenye muziki ni ladha
ya muziki mzuri 'audio' ndiyo inaweza kuuza muziki huo japokuwa ni
vizuri muziki ukiwa na video.
“Mimi naamini kitu cha
kwanza kwenye muziki ni audio, Ndiyo maana unaona watu zamani tulikuwa
tunapiga audio strong na ilikuwa inauza..., Watanzania wameshaacha
ushamba wa picha ndio maana hata ukitoa video kali kama audio sio nzuri
ngoma inakufa” Amesema Joh Makini.
Katika hatua nyingine Joh Makini
amefunguka kuhusu suala la mashabiki kutumiana nyimbo kupitia mitandao
na kwamba watumie njia sahihi ili kusapoti kazi za wasanii
wanaowakubali.
“Watu waache kutumiana audio
kwenye Whats App au makundi halafu kwenye interview unakuta mtu
anaulizwa album lini, kama umeshindwa kununua ngoma moja mtandaoni
utawezaje kununua album?” Joh Makin alisema kwa mtindo wa kuhoji.
No comments:
Post a Comment