Wahalifu Wanne Wauwawa Katika Mapambano Na Polisi Kibiti
Jeshi
la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa
miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga,
Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa
katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akielezea
tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu
Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya
Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi
itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria
walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo
wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na
kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas
alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na
mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa
kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia
wakiwa wanapelekwa hospitali.
“Katika
tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine
mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii
ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo
inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi
tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.
Aidha
Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo
hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya
jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na
wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile
amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu
wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa
ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao
kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Simon Sirro.
No comments:
Post a Comment