Trending News>>

Vitu 15 ameviongea Rais JPM akiwa ziarani Mkoani Pwani leo

Leo June 20, 2017 Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi ya sikuu tatu mkoani Pwani ambako atazindua viwanda vitano pamoja na mradi wa maji wa mto Ruvu. Akiwa kwenye siku ya kwanza eneo la Bwawani Rais JPM amezungumza na wananchi kutaja vitu 15 ambavyo serikali yake inavifanya na itafanya.
Nimekukusanyia hapa chini unaweza kuvisoma.
1. 'Mkionana wachache wanalalamika mujue Magufuli anafanya kazi, mkiona wachache wanalia wanasema Magufuli anatumbua semeni tumbua'-@MagufuliJP
2.Sizungumzii wana CCM ninazungumzia Watanzania wote tatizo alilonalo mwana CCM analo wa ACT, wa CHADEMA au wa CUF' - Rais @MagufuliJP 
3. 'Tanzania ni ya pili kwa vivutio vya kitalii duniani ikiongozwa na Brazil, lakini vivutio hivi haviwanufaishi Watanzania' - Rais @MagufuliJP
4. 'Tanzania tuna kila kitu lakini angalieni sehemu tulipo, kuna mahali tulikosea na lazima tuparekebishe' - Rais @MagufuliJP
5. Tumelipa madeni ya serikali ambayo ilikuwa inadaiwa na wafanyakazi, tunataka tufike mahali tusiwe tunadaiwa kabisa' - Rais @MagufuliJP
6. 'Nimeongea na Waziri Mkuu wa Ethiopia ameniambia atatuma wataalam watusaidie kujenga bwawa la kuzalisha umeme wa kutosha' - Rais @MagufuliJP
7. 'Mimi nachukia sana wezi awe mwizi wa ndani au wa nje mwizi ni mwizi tu na wataula wachuya awamu hii' - Rais @MagufuliJP
8. 'Kibiti nawaambia kwenye awamu hii hawatapita najua walikuwa wachache na moto wameshaanza kuuona narudia tena hawatapita' - Rais @MagufuliJP
9. 'Tunanunua ndege na kujenga reli ya kisasa kwa kuwa sisi Tanzania ni matajiri ni lazima tuishi kitajiri tajiri' - Rais @MagufuliJP 
10. 'Tumenunua ndege sita mpya hadi sasa zipo mbili zinazofanya kazi, nyingine inakuja na nyingine tatu zitakuja mwakani' - Rais @MagufuliJP
11. 'Tunaochelewesha maendeleo ya Kibiti na Rufiji ni sisi wenyewe, hakuna mtu atakayekwenda kuwekeza sehemu watu wanauana' - Rais @MagufuliJP
12. 'Mimi nimeshaalikwa kwenye nchi zaidi ya 50 lakini siendi mimi humu humu kwanza tunyooshane najua nikitoka watu watalala' - Rais @MagufuliJP
13. 'Kama Halmashauri haiwezi kujenga barabara waseme wasipewe fedha ili zibaki serikali kuu tujenge wenyewe barabara zetu' - Rais @MagufuliJP
14. 'Nataka kila kiongozi kwa nafasi yake ajitafakari anasaidiaje wananchi masikini na ukiona hupati jibu jiondoe mwenyewe' - Rais @MagufuliJP
15. 'Niliamua kwa makusudi kabisa Wizara ya TAMISEMI iwe chini ya Rais kwa sababu nataka kuisimamia mwenyewe kama Waziri' - Rais @MagufuliJP
Powered by Blogger.