Usaliti wa Manchester United ulimfanya “Dinho” aende Barca
Hakika Ronaldinho Gaucho ni mchezaji ambaye kila klabu
inatamani angekuwa mchezaji wao kutokana na ubora aliokuwa nao Mbrazil
huyo katika kipindi chake.
Mwaka 2003 inasemekana Joan Laporta ambaye ni mwanasiasa nchini
Hispania lakini pia alikuwa raisi wa klabu ya Barcelona alimsaini
Ronaldinho baada ya Manchester United kumzunguka.
Ilikuwa hivi, klabu ya Manchester United walikubaliana na Laporta
kwamba akishinda uchaguzi Barcelona baasi watawauzia David Beckham
aliyekuwa katika kiwango kizuri.
“Ilikuwa tumchukue Beckham,Ronaldinho au Henry na United wakatuambia
watatupa Beckham lakini hawakufanya hivyo wakatuzunguka wakamuuza Real
Madrid” alisema Laporta.
Kumbuka wakati Barcelona wanamtaka David Beckham na kuahidiwa kuuziwa
na United, Manchester United nao kipindi hicho walikuwa wakihitaji
kumsajili Ronaldinho ambaye kipindi hicho alikuwa PSG.
Manchester United tayari walishatuma ofa kwenda PSG na ilionekana
wanakwenda kumchukua Ronaldinho lakini Barcelona waliamua kulipiza
walichofanyiwa na Manchester United kwa Beckham.
Barcelona waliamua kutuma ofa kubwa zaidi kwa klabu ya PSG ambayo kwa
haraka haraka ilikubaliwa na wakamnunua Ronalinho huku United wakibaki
wanashangaa shangaa.
Rinaldinho alipojunga na Barcelona ndio jina lake lilizidi kuwa kubwa
na baada ya United kushindwa kufanya usajili huo walihamia kwa
Cristiano Ronaldo ambaye naye alifanya vizuri klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment