Trending News>>

Taifa Stars kukipiga na Angola leo Afrika Kusini

 
 Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kuingia uwanjani hii leo kuvaana na Angola kwenye mechi ya pili ya mashindano ya Cosafa yanayoendelea huko nchini Afrika Kusini.

Stars itaingia uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu nzuri katika mchezo uliopita baada ya kuchomoza na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa ya Malawi Jumapili ya Juni 25, mwaka huu katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa).

Mchezo wa Stars dhidi ya Angola unatarajiwa kuanza majira ya saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.


No comments:

Powered by Blogger.