Singida United yamvuta Batambuze
Klabu ya Singida United ambayo nayo
inaendelea na usajili katika kuimarisha kikosi chake ambacho msimu mpya
wa Ligi Kuu Bara kitakuwa kikicheza na timu mbalimba za Ligi Kuu baada
ya timu hiyo kupanda daraja na kuingia Ligi Kuu.
Singida
United wamekwea pipa mpaka nchini Kenya katika klabu ya Tusker FC na
kumchukua kiungo wa kimataifa Shafik Batambuze raia wa Uganda ambaye
anakipiga katika klabu hiyo ya Kenya.
Tusker FC wamethibitisha kiungo wao huyo kujiunga na klabu ya Singida United kwa mkataba wa mwaka mmoja, lakini pia Singida United pia wamethibitisha taarifa hizo baada ya kupost taarifa ambayo imewekwa na klabu ya Tusker FC kuonyesha kuwa mchezaji huyo atatua Singida kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
Batambuze anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Singida United baada ya kumkosa aliyekuwa goli kipa namba moja wa Azam FC, Aisha Manula.