Serikali yatoa kibali cha kuajiri watumishi 15000 kuziba nafasi za watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki.
Waziri
wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki
amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya
kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti
feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu
nafasi hizo zitajazwa.
Mh.Kairuki
amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la
mbunge wa viti maalum Iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya
ujazwaji wa nafasi hizo ambapo amekiri upungufu huo umesababisha
usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia
wananchi kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.
Katika
hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha
Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai
kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika
Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano
Mh.Edwin Ngonyani amesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza
bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo
bandari ya Dar es Salaam.
Mh.Ngonyani
amesema kuwa tayari serikali imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa
gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu
zaidi ya shilingi bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.
No comments:
Post a Comment