Trending News>>

Serikali ituvumilie - Sumaye


Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kuitaka serikali ya awamu ya tano iwavumilie na itambue kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM inavyofanya kazi zake.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye
Sumaye aliyasema hayo jana baada ya jeshi la polisi kuzuia msafara wao ambao ulikuwa na lengo la kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.
"Hili si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM kwa mfano hata Pole Pole anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna tatizo ila inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza mapambano, tunadhani huu ni uonevu tu unaendelea wa kujaribu kuwafanya watu wengine wajisikie kwamba hawana uhuru na nchi yao hili nafikiri si jambo jema, serikali tunaomba ituvumilie ijue kwamba CHADEMA pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM wanavyofanya kazi kwa hiyo mambo ya kuandamwa CHADEMA kila mahali inatusikitisha sana" alisema Sumaye
Mbali na hilo Sumaye anasema vitendo hivyo vinavyofanywa kwa viongozi wa CHADEMA ni kutaka kukatisha tamaa jitihada zozote zinazofanywa na viongozi wa chama hicho hivyo anadai ni kitu ambacho hakiwezi kuvumilika.
"Kwa jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani wataleta vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye kazi zao hapa hakuna siasa zozote tunazofanya, tunakagua miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea kwenye halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na sisi tunataka kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale ambayo CHADEMA imewaagiza kufanya katika Ilani yake. Na miradi hii ni kwa wananchi wote" alisisitiza Sumaye   
Powered by Blogger.