Rais Magufuli Atoa Ekari 65 za Magereza na Kuwapa Wananchi
Rais John Magufuli amewapa wakazi wa Bagamoyo, eneo la Magereza lenye ukubwa wa heka 65.
Rais
Magufuli amechukua uamuzi huo leo (Alhamisi) wakati akihutubia katika
mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.
Alichukua
hatua hiyo baada ya wanawake waliokuwa wamebeba mabango, kumtaka awape
eneo lao kwa kuwa ni wazaliwa wa Bagamoyo, ni wajane na wana uhaba wa
maeneo ya biashara.
“Akina
mama mnaokaa huko na akina baba nimewapa hilo eneo lakini natoa
tahadhari, mpaka wenu sasa ni barabara, msivuke mkaenda upande ule,”
amesema.
Amelitaka Jeshi la Magereza kufanya mabadiliko katika hati ili eneo hilo liwe la wananchi.
No comments:
Post a Comment