PICHA: Ben Pol Amekutana na Ebitoke Leo Juni 23
Sasa leo June 23, 2017 kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha
akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa
kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.
“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona
kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi
fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba
kwa Mhusika?
“Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa
sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao,
Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu
duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.
“Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza
sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini
huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na
nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako 🙏🏽😍. Nakushukuru
sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST 💪🏾!!@ebitoke
#blessed🙏🏽” – Ben Pol.
No comments:
Post a Comment