Pesa zamfukuza Saida kwenye muziki
Mkongwe wa muziki wa asili
wenye ladha ya bongo fleva, Saida Karoli amefunguka na kusema kwamba
ukosefu wa pesa na mapromota waongo ndicho kitu pekee kilichomfanya
apotee katika ramani ya muziki nchini.
Saida
amefunguka hayo baada ya ujio wake mpya kwa kuachia video inayokwenda
kwa jina la 'Orugambo' na kuongeza kwamba aliamua kurudi kijijini kwao
baada ya kukosa muelekeo maalumu.
"Nisingeweza kufanya kitu
chochote bila kuwa na pesa, mapromota waliniangusha sana kipindi kile
kitu ambacho kilinifanya nipotee. Sasa hivi nimerudi nashukuru Mungu
japo sijapata uongozi lakini kuna watu wameamua kujitolea ili kipaji
changu kisipotee", Saida alifunguka
Kuhusiana na suala la kutengeneza muziki
mzuri, Saida amesema muziki wake unaonekana kuwa mzuri kwa sababu
anatumia vitu vya asili katika kuutengeza .
"Muziki wangu mimi siandiki
kabisa mashairi kwenye karatasi, huwa natunga mashairi wakati nikiwa
studio napiga ngoma za asili. Huwa sipendi vionjo vya ngoma
vinavyotengenezwa na kompyuta, na hiyo ndiyo sababu muziki wangu unakuwa
na ladha ya tofauti"' Saida alizidi kufunguka.
Saida amewahi ametamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Maria Salome, Kizunguzungu na nyinginezo nyingi.
No comments:
Post a Comment