Nafasi za kazi zilizoachwa wazi kujazwa....
VIBALI vya kuajiri watumishi wengine baada wengi kuondolewa kutokana na
sakata la vyeti feki vinaendelea kutolewa ili kuziba mapengo yao.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaziba mapengo ya watumishi hasa wa afya walioondolewa kutokana na sakata la kuwa na vyeti feki. Majaliwa alisema ni kweli uhakiki umefanyika na serikali ikabaini kwamba baadhi ya wafanyakazi walikuwa na vyeti feki. Alisema wengine walikuwa na vyeti ambavyo ama vinatumika mara mbili kwa watu zaidi ya mmoja.
“Lakini wapo waliobainika kwamba kuna utata katika majina katika vyeti hivyo, ambao ndio waliruhusiwa kukata rufaa na leo ndio siku ya mwisho ya kuangalia tatizo hilo,” alisema. Alisema baada ya uhakiki kukamilika, Rais John Magufuli tayari ameshatoa vibali vya kuajiri zaidi ya watumishi 50,000 na anaendelea kutoa na kinachoangaliwa zaidi ni kuziba mapengo ya watalaamu kwenye sekta mbalimbali.

No comments:
Post a Comment