Mlinzi aliyevunja, kutishia Kuua na kumbaka Binti wa Miaka 16 afungwa miaka 30
Mahakama
ya Wilaya ya Mlele imemuhukumu mlinzi wa Sekondari Ilela, George Sikoki
kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya
kumbaka mtoto wa umri wa miaka 16.
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi Mfawidhi Teotimus Swai baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.
Mwendesha
mashtaka, Baraka Hongoli alidai katika ushahidi mahakamani hapo kuwa,
mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 27 saa 7:30 usiku.
Alidai
Sikoki ambaye ni mlinzi wa shule hiyo iliyopo tarafa ya Inyonga
wilayani hapa alitenda kosa hilo wakati ambao wazazi wa mtoto huyo
wakiwa safirini naye alikuwa akilala peke yake.
Upande
wa mashtaka ulidai mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa mtoto huyo na
kuvunja mlango kisha kumtishia kumuua iwapo angepiga kelele hivyo
kumbaka na kutokomea kusikojulikana.
Ilielezwa
mahakamani kuwa binti huyo akiwa na maumivu makali, huku akitokwa damu
sehemu za siri alijikongoja hadi kwa jirani na kutoa taarifa ndipo
alipopelekwa hospitali kwa matibabu.
Hongoli
alidai baada ya mshtakiwa kukamatwa alikiri kosa hilo kwa maandishi
wakati akihojiwa kituo cha polisi, lakini alipofikishwa mahakamani
alikana.
Upande
wa mashtaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita akiwamo daktari
kuthibitisha shtaka hilo ambapo waliithibitishia mahakamani bila kuacha
shaka
No comments:
Post a Comment