Trending News>>

Mke na Mume wafariki dunia Pamoja

Watu wawili ambao ni mtu na mkewe wamefariki dunia wakati wakipata matibabu kwenye zahanati baaada ya kunywa chai inayohofiwa kuwa ilikuwa na sumu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amezungumza na wanahabari leo na kuthibitisha kuwa wanandoa hao wamepoteza maisha baada ya kunywa chai hiyo.
“Walikunywa chai hiyo jana saa 7.00 mchana katika Kijiji cha Baga, Tarafa ya Mgwashi wilayani hapa,” amesema.
Amesema majirani wa  wanandoa hao walishtuka  baada ya kuona muda unakwenda bila jirani zao hao kutoka nje ndipo walipoingia na kukuta wamelala huku wakiwa hawajitambui  ndipo wakawakimbiza katika zahanati ya Baga.
Kamanda Wakulyamba amewataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni Rajab Ali Rajab (72) na mkewe Amina Rajabu (62) huku mpwa wao Adamu Said(12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mashine akinusurika.
Amesema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo hicho ingawa taarifa za awali kutokana uchunguzi wa daktari unaonyesha walikunywa chai inayodhaniwa kuwa na sumu.
“Tunachunguza kujua kama sumu hiyo ilitoka wapi na waliwekewa na nani na kwa sababu zipi hatimaye ili kujiridhisha na kama litakuwa tukio lakuwekewa sumu hiyo tutahakikisha tunawakamata walioshiri.” amesema Wakulyamba.

No comments:

Powered by Blogger.