Marekani yatishia kuishambulia Syria, yasema matumizi ya silaha za kemikali hayakubaliki
Marekani
imeionya Syria dhidi ya matumizi ya silaha zenye kemikali ambazo
inatarajia kuzitumia dhidi ya kikundi cha wanamgambo wa Islamic State.
Aidha,
taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imemuonya rais wa Syria,
Bashar al Assad kuwa endapo atatumia silaha zenye sumu basi Marekani
itamchukulia hatua kali zikiwemo kuishambulia nchi hiyo.
Imesema
kuwa shambulio lolote litakalofanywa na Syria lenye silaha zenye sumu
dhidi ya wanamgambo wa Islamic State litasababisha vifo vya raia
wasiokuwa na hatia.
Hata
hivyo, Marekani imeongeza kuwa iko Syria kwaajili ya kukabiliana na
wanamgambo wa Islamic State lakini imeionya Syria kuwa kama itafanya
shambulizi lolote lenye silaha zenye sumu itakiona cha moto.
No comments:
Post a Comment