Kama ulichukuliwa mifugo yako na serikali, fuata utaratibu huu kurejeshewa
Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Paje Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ Haji Omar Kheri amesema utaratibu wa kuwapata tena wanyama hao kwa wamiliki wa mifugo hiyo ni kuchukua barua katika Shehia anayofugwa mnyama husika na kuiwasilisha barua hiyo ya utambuzi katika Manispaa yao
Hata hivyo Haji amesema lazima mfugaji alipie gharama za utunzaji wa wanyama hao kwa kipindi chote alichokaa mnyama katika hifadhi ya serikali na atakabidhiwa mnyama wake akiwa amewekwa alama maalum kwa lengo la udhitibi wa kurudi tena kuwaweka wanyama hao katika maeneo yasiyoruhusiwa kufuga.
Aidha amefafanua kuwa endapo mnyama huyo aliyeekewa alama atakamatwa tena katika maeneo yasiyoruhusiwa mnyama huyo atakuwa mali ya Serikali na taratibu husika za kuuzwa zitafuatwa.