Kagera Sugar yapinga usajili wa Mbaraka Yusuph, yapanga kupeleka madai Tff
Siku mbili baada ya Azam kutangaza kumsajili mshambuliaji Mbaraka
Yusuph, uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar alikotokea mchezaji huyo
umeibuka na kupinga usajili huo, huku ukipanga kupeleka madai yake
TFF.Kagera Sugar inapinga usajili huo kwa madai kuwa bado mchezaji huyo
ana mkataba na wakata miwa hao wa Kagera.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, uongozi wa klabu hiyo ukiongozwa na meneja wake, Mohamed Hussein hivi sasa unaelekea katika Shirikisho la Soka Tanzania TFF kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko rasmi.
Mbaraka ambaye amefunga mabao 12 katika msimu uliomalizika wa ligi, amekuwa akiwaniwa pia na Yanga, huku Kagera wakitaka kumbakiza mikononi mwao, lakini Azam wamefanikiwa kunasa saini yake kwa mkataba wa miaka miwili.

No comments:
Post a Comment