Jina ZUZU Lamkera aliyewaikuwa WAZIRI MKUU WA AWAMU YA NNE Mh. Mizengo Peter Pinda
WAZIRI
Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amesema anafarijika kuona mchakato wa
kubadilisha jina la kijiji cha Zuzu umeanza kwa kuwa jina hilo halina
ustaarabu kulingana na maana yake halisi.
Alisema
sasa wanakwenda kupata jina linaloendana na eneo hilo ambalo wanaishi
wachapakazi wengi. Shamba la Pinda lililoko kijiji cha Zuzu ni moja ya
miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru juzi na kuwawezesha wakimbiza
Mwenge kitaifa kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika
shamba hilo ambalo pia linatajwa kuwa shamba darasa kwa sasa.
Alisema licha ya mafanikio mengi ambayo yamepatikana kilio chake ni jina la kijiji kuwa halina ustaarabu masikioni mwa watu.
”Zuzu
maana yake ni mpumbavu, silipendi jina hilo, sijui walitoa wapi
nimekwenda kwenye mtandao nakuta jina ni Zinje kila nikiuliza sipati
jibu lini walitubaini sisi ni mazuzu watu wazuri huku tunafanya kazi
tunajiendeshea maisha yetu,” alisema
“Nikamwambia
mkuu wa mkoa jina hili si letu ila wametubambikiza tu. Hoja tunayo
nadhani serikali imetusikia na tutapata jina ambalo linaendana na eneo
hili,” alisema.
Kwa
upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour
amewataka viongozi nchini kutekeleza kwa vitendo sera, mipango na
mikakati ya kukuza uchumi badala ya kuhubiri na kuhimiza kwa wananchi
bila wao kuonesha mfano.
“Huu
ni mfano ulio bora unaopaswa kuigwa na kila kiongozi mikakati ya kukuza
uchumi katika nchi inatakiwa kutekelezwa kwa vitendo,” alisema.
Awali
akitoa maelezo kuhusu shamba hilo, mke wa Waziri Mkuu mstaafu Pinda,
Tunu Pinda alisema harakati za kuanzisha shamba hilo zilianza mwaka 2001
na shamba hilo lina ukubwa wa ekari 60.
Alisema
shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika shamba hilo ikiwemo
kilimo, ufugaji na huzalisha gesi ya asili ya biogas kwa ajili ya
nishati ya kupikia na taa.
Alisema
shamba hilo limekuwa likitumia mbolea ya samadi katika kilimo. Pia
alisema shamba hilo lina mizinga 403 ya kisasa ambapo katika msimu wa
mavuno uliopita kiasi cha tani 7.5 za asali zilipatikana. ‘’Bidhaa
zinapatikana dukani kwa nembo ya Pinda Honey” alisema.
No comments:
Post a Comment