Trending News>>

Hadithi hii ya Gabriel Jesus ikutie moyo kufikia malengo yako


Maisha ni juhudi na kupamban, bahati katika maisha haipo kwani hata mungu alitupa maarifa na vipaji ili tuvitumie katika kufanikisha malengo yetu ya kila siku, na hata hiyo “bahati” huwatembelea wanaopenda kujaribu.
Maneno hayo katika aya ya kwanza yanalandana na historia ya mwanasoka tishio katika klabu ya Manchester City Gabriel Jesus ambaye sasa sio tu ni tajiri bali ni kati ya wacheza na nyavu wanaozungumziwa sana Uingereza.
Jesus ambaye amesajiliwa kwenda Manchester City kwa ada ya £32m miaka mitatu iliyopita hakuna hata mtu mmoja ambaye alidhani anaweza kuwa na maisha aliyonayo hivi sasa ya kuendesha magari mazuri na kuishi katika nyumba nzuri.
Miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 17 tu ilimbidi afanye kazi ya ziada ili kupata kipato, Jesus aliamua kuwa mpaka rangi mitaani mjini Sao Paulo ambapo alifanya kazi hiyo katika mida wa ziada akitoka mazoezini.

Lakini hii haikumzuia Jesus kufukuzia ndoto zake kwani katika muda wake wa ziada alikwenda mazoezini kama kawaida na kuoambana uwanjani ili kutimiza ndoto zake ambazo zilikuwa katika soka.
Miaka mitatu sasa Jesus yuko kwenye kilele cha ndoto zake, hii inatufunza nini?kesho yako bora inaanza na leo,haijalishi ni mangapi unayoyapitia hupaswi kukata tamaa,pambana na amini katika ndoto zako na kila kitu kitakuwa sawa.

No comments:

Powered by Blogger.