Gabo ajinadi kuikomboa filamu
Muigizaji Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’
amefunguka kwa kudai kwamba ameamua kujitolea kufa na kupona ili
kunusuru tasnia ya filamu isonge mbele kwa kutumia Teknolojia ya simu
ambayo itawasaidia Watanzania kupata filamu bure na kwa urahisi.
Gabo
amedai hayo wakati akizindua filamu yake ya 'Kisogo' kwamba ameamua
kutoa sehemu ya maisha yake ili kuikomboa tasnia ya filamu ambayo
imeonyesha kupoteza imani kwa mashabiki wa filamu nchini Tanzania kwa
kutumia akili alizojaaliwa pamoja na kipaji chake kwa kadri
atakavyopatiwa ushirikiano.
“Mimi nimeamua kuikomboa
tasnia ya filamu. Haiwezekani nyimbo zinapata heshima kubwa kuliko
filamu, wakati filamu inaweza kuelezea kwa upana jambo na
kueleweka. Unajua kuna wakati unafika lazima ukubali maneno ya watu
ambao ni mashabiki wetu. Kwahiyo mimi binafsi nimeanza kutoa filamu fupi
ambazo zitakuwa zikipatika katika App ya Uhondo, nimeanza na Kisogo,
hizi filamu zimezingatia ubora ya kila kitu kuanzia picha, sauti,
wahusika yaani kila ambacho kilikuwa kinazungumzwa mtandaoni kuhusu
filamu,” alisema Gabo
Aliongeza,”Kwa sasa filamu fupi
zitapatikana kupitia mtandao wa Uhondo na kila mtu mwenye simu ya
mkononi ataweza kuzipata, sehemu ya 1 bure na sehemu ya pili itakuwa
ikichangiwa pesa kidogo ili kuweza kuzalisha kazi nyingi zaidi. na
kwamba malengo ya kufanya hivyo ni ili kila mtanzania aangalie filamu
hizo na baadaye mambo yakikaa sawa zitakuwa zikipatikana bure kabisa