Trending News>>

Farid Musa anazisubiri dakika 90 zitakazoamua acheze La Liga 2017/18


Good news iliyotufikia usiku wa June 22 2017 kuhusiana mtanzania anayecheza soka Hispania Farid Musa kuhusiana na timu yake ya Tenerife inayocheza Ligi daraja la kwanza Hispania maarufu kama Segunda, inaweza kupanda kucheza Ligi Kuu Hispania msimu wa 2017/18.

Ushindi wa goli 1-0 wa Tenerife dhidi ya Getafe umeiweka Tenerife katika nafasi nzuri ya kukaribia kucheza LaLiga msimu ujao, hivyo hiyo inaweza kuwa ni good news kwa mtanzania Farid Musa kama watafanikiwa kucheza La Liga maana ndio atakuwa mtanzania wa kwanza kucheza Ligi hiyo.

Tenerife kwa sasa wanasubiria mchezo wao wa marudiano wa play off dhidi ya Getafe, ili ijulikane kama wamefuzu au la kwa maana baada ya leo kucheza nyumbani, Jumamosi ya June 24 watacheza katika uwanja wa ugenini, watahitaji sare au ushindi kupanda daraja na kucheza LaLiga.

No comments:

Powered by Blogger.