Walimu waliomsababishia mwanafunzi kifo wasakwa
Siku moja baada ya vyombo vya habari kuripoti Kisa cha Mwalimu Mkuu
kumfungia mtoto katika chumba cha hazina, mwanafunzi Daudi Kaila wa
shule ya msingi Matwiga na kusababisha kifo chake, Mkuu wa Wilaya ya
Chunya Rehema Madusa ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama
wilayani humo kuwasaka na kuwatafuta walimu hao popote walipo.
Mkuu wa Wilaya huyo alipofika katika shule hiyo pamoja na kuzungumza na wananchi alitoa pole na kuwahakikishia wananchi kuwa haki itatendeka kwa yeyote aliyehusika.
“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana hakikisheni mnawatafuta watu hawa, hakikisheni mnawatafuta waklimu wote waliohusika kwa kushirikiana na wananchi,” alisema Madusa.
Kwa upande wa Jeshi la polisi wilayani Chunya limewaahidi wananchi kuwa haki itatendeka.

No comments:
Post a Comment