Trending News>>

Vyakula vinavyoongoza kwa kuongeza akili kwenye ubongo


Katika mwili wa mwanadamu hakuna kitu chenye umuhimu mkubwa kama ubongo, ubongo ndio ambao humsaidia mwanadamu katika kufanya mambo mbalimbali, hata hivyo inaelezwa ya kwamba ubongo wa mwanadamu ndio humfanya mwanadamu kuonekana hivyo alivyo.

Hivyo inaelezwa ya kwamba ili mwanadamu aweze kuongeza akili, katika kufikiri na kutenda mambo mbalimbali anatakiwa kula vyakula vifuatavyo:

1. Mafuta ya samaki.
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama sangara na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

2. Ulaji wa mbegu za maboga.
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama
karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, huweza kusaidia kuweza kuongeza akili.

3.Pilipili kali.
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa. Hivyo unaweza ukatumia pilipili kali kama vile pilipili kichaa, pilipili mbuzi kwani hizo ni mifano ya pilipili kichaa.

4.Nanasi.
Utumiaji wa nanasi pia ni miongoni mwa matunda ambayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongezea uwezo wa kiakili.

5. Nyanya
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

6.Karanga
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

7. Mayai ya kienyeji.
Mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

No comments:

Powered by Blogger.